
SIKU
chache baada ya kuanza rasmi maisha ya ndoa, staa wa fi lamu za
Kibongo, mwanadada Shamsa Ford ameibuka na kueleza wazi kuwa anajutia
kuchelewa kuolewa, kwani maisha ni ya kupendeza kuliko alivyodhani.
Akizungumza
na Za Motomoto News, Shamsa alisema maisha ya ndoa ni matamu na
anajiuliza na kujilaumu kwa nini alichelewa, hivyo anamshukuru Mungu kwa
kumpa Chidi Mapenzi, kwani ni ndoto yake ya muda mrefu ya kupata mume
bora ili wajenge familia bora.
“Ndoa
ni tamu sana jamani kuliko maisha ya kuwa singo, najiuliza sijui
nilikuwa nachelewa wapi kuingia humu, naamini tutaendelea kupendana na
mume wangu hivihivi mpaka mwisho wa maisha yetu kwani kabla ya kuoana
tulikaa kwenye uchumba kwa muda wa miezi nane na tabia zetu tukaona
zinaenda,” alisema
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon