CHAMA
Cha Mapinduzi (CCM), kimeitaka Serikali kuhakiki akaunti na mali za
Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT) na wenzake waliokuwa katika
kamati za fedha za Bunge, ili kubaini kama zinalingana na kipato
walichokuwa wakipata.
Msemaji wa chama hicho,
Christopher Ole Sendeka, amesema hayo jana alipozungumza na waandishi wa
habari, akimuhusisha Kiongozi huyo Mkuu wa ACT na tuhuma za ufisadi wa
Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), alipokuwa Mwenyekiti wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC).”Nilikuwa najiuliza hivi
chuki ya Zitto kwa Serikali ya Awamu ya Tano, inayopambana na mafisadi
imetoka wapi wakati yeye alikuwa anasimamia mashirika hayo.
“Miongoni mwa taasisi
hizo alizokuwa akisimamia na baadhi ya marafiki zake ndiyo hao
walionunua hekari moja kwa Sh milioni 800, wakati ilikuwa ikiuzwa kwa Sh
milioni 25 na walikuwa wamejificha kwa maslahi binafsi,” alisema katika
ofisi ndogo za Makao Makuu, Lumumba Dar es Salaam.
NSSF ndiyo iliyonunua
hekari 20,000 Kigamboni jijini Dar es Salaam kwa Sh milioni 800 kwa kila
hekari, badala ya Sh milioni 25 na kujikuta katika hatari ya kupoteza
Sh bilioni 270, katika mradi wa ujenzi wa mji wa kisasa wa Dege Eco
Village.
Kutokana na tuhuma hizo
za NSSF zilizoibuka upya katika kamati ya PAC wiki hii, Sendeka alisema
ni vema Serikali ikague kuona kama akaunti za viongozi wa zamani wa
kamati hizo, maisha yao na mali walizonazo, zinafanana na mapato halali
waliyokuwa wakilipwa.
Alisema alikuwa
anaangalia msukumo wa ghafla na mapenzi ya akina Zitto waliyokuwa
wanayapata kwa nchi, kumbe ilikuwa ni kichaka cha kuficha baadhi ya
maswahiba zao wasichukuliwe hatua.
Aliwahakikishia wananchi
kuwa Serikali ya Rais Magufuli haina nia ya kurudi nyuma katika jambo
lolote na kuwa itasonga mbele huku akiamini kuwa Serikali iliyochaguliwa
na watu haiwezi kufa.
“Tunahakika Serikali ya
Magufuli iliyopata ridhaa ya kutumikia watu, haitafutika kwa kelele za
mlango wa baadhi ya makuwadi na watu waliolipwa kuchafua taswira ya
Tanzania,” alisema.
Aliongeza kuwa Serikali
hiyo itaendelea kushughulikia wakwepa kodi pamoja na kuchunguza mambo
aliyoanzisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipokuwa bandarini.
Kauli ya Zitto
Akizungumzia tuhuma hizo, Zitto Kabwe alisema hana muda wa kujibu alichoita kuwa ni porojo na vioja vya Sendeka.
Alifafanua kuwa CCM ni
chama dola na kuna taasisi nyingi za uchunguzi za Serikali, ikiwemo
Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) na Mkurugenzi wa
Mashitaka ya Jinai (DPP) na kushangaa kwa nini vyombo hivyo havisemi,
aseme Sendeka?
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon