Mganga
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Grace Magembe akiongea na wakazi wa
Buguruni kabla ya kumkaribisha mkuu wa mkoa Mh. Paul Makonda
Mkuu wa Mkoa wa Dar, Makonda alipokuwa akiongea na wananchio na kuhimiza kuhusu matumizi ya dawa za kujikinga na magonjwa hayo.
Bibi mkazi wa Buguruni Shell naye akinywa dawa ili kuilinda afya yake dhidi ya Magonjwa hayo Hatari.
WAKAZI
wa Jiji la Dar es Salaam wametakiwa kunywa dawa za kujikinga na
magonjwa ya mabusha, matende, usubi na minyoo ambazo zitawapa kinga
dhidi ya magonjwa hayo.
Wito
huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, alipokuwa
akizungumza leo eneo la Buguruni Shell katika uzinduzi wa zoezi hilo la
unywaji wa dawa litakalochukua siku tano ambapo amesema wagonjwa
watakaopatikana na matatizo watafanyiwa upasuaji.
“Tumeandaa
vituo vya afya Pugu na Mbweni Mission ambako upasuaji utakuwa
unaendelea tukishirikiana na madaktari kutoka hospitali ya Muhimbili,”
alisema Makonda.
Ameongeza
kuwa zoezi la upasuaji litaendelea hadi mwezi wa 12 mwaka huu, ambapo
hadi sasa zaidi ya wagonjwa 104 wamefanyiwa upasuaji.
“Zoezi
hili tumelipa kipaumbele ili kuokoa nguvu-kazi ya taifa, tumeandaa
vituo zaidi ya 281 kwa ajili ya zoezi hili hivyo wanaume kwa wanawake
wajitokeze kumeza dawa hizi,” alisisitiza akiwataka pia wananchi kupuuza
maneno ya mitaani kwamba dawa hizo zina madhara.
Aliwataka pia waendeleze zoezi la usafi ili kuepuka mazalia ya mbu ambapo ni vigumu kuwatambua mbu wanaoeneza ugonjwa huo.
Wizara
ya Afya na Ustawi wa Jamii imeendesha zoezi hili kuanzia mwaka 2009
ambapo kwa Mkoa wa Dar es Salaam linatarajiwa kuwafikia wananchi zaidi
ya milioni nne ili kuwakinga dhidi ya magonjwa hayo.
Habari/Picha: Hilaly Daudi/GPL
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon