Baada
ya kilio cha muda mrefu kutoka kwa mashabiki waliotamani kuona Diamond
Platnumz na mwanadada Lady Jay Dee wakifanya kazi pamoja, wakali hao wa
bongo fleva huenda wakaja na 'collabo' ya hatari, siku chache
zijazo.Hatua hiyo inatokana na msanii Diamond kufunguka kuwa hakuna
sababu yoyote inayowakwamisha kufanya kazi ya pamoja, isipokuwa muda na
ratiba zao kubana.
Dangote ametoa kauli hiyo hivi karibuni alipotembelea ofisi za EATV, na kukutana na maswali mbalimbali ikiwemo sababu za wao kutofanya kazi ya pamoja licha ya mashabiki kuitamani 'collabo yao.
"Siku si nyingi tutafanya kazi pamoja na Jay Dee, kilichotukwamisha ni ratiba zetu, lakini pia nilikuwa sijafikiria hilo, ila sasa kwa kuwa mashabiki wamekuwa wakiomba kila mara, nitawasiliana naye, na tutafanya kazi ya pamoja muda mfupi ujao, hakuna sababu nyingine tofauti na kubanwa na kazi nyingi, pamoja na ratiba zetu kutoendana"
Kuhusu ni lini mashabiki wategemee kazi hiyo, Dangote alisema kuwa hawezi kuahidi tarehe, lakini ana uhakika 'collabo' hiyo inakuja.

Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon