MBUNGE wa Ukonga Mh. Mwita Waitara Akamatwa na Kushikiliwa na Polisi kituo cha Polisi Chang'ombe

Mbunge wa Ukonga Mh. Mwita Waitara akamatwa na kushikiliwa na Polisi kituo cha Polisi Chang'ombe, Temeke.

Mh. Waitara amekamatwa muda mfupi uliopita katika eneo la UVIKIUTA alipokuwa amefuatilia mgogoro wa muda mrefu wa ardhi kati ya wananchi wa eneo hilo na kigogo mmoja wa serikali anayetaka kupora ardhi hiyo na kuwahamisha wananchi kwa nguvu.

Leo asubuhi wananchi wa UVIKIUTA wamekumbwa na bomoa bomoa iliyokuwa inasimamiwa na askari wa jeshi la Polisi kutoka Temeke.

Mh Waitara ambaye pia ni Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Kivule linakopatikana eneo hilo la UVIKIUTA ambalo lipo mpakani mwa wilaya za Ilala na Temeke (Kivule-Ilala na Mbande-Temeke), alifika eneo hilo kufuatilia bomoa bomoa hiyo ndipo Polisi wakamkamata na kumpeleka Chang'ombe.
Previous
Next Post »