Ommy Dimpoz: Nilivurugana na Diamond Kisa Wema Sepetu, Aanika Bifu la Kiba na Diamond

STAA wa Bongo fleva hapa nchini, Ommy Dimpoz anayetamba na ngoma yake ya ‘Kajiandae’, amefungukia bifu lake na msanii mwenzake, Diamond Platinumz kuwa chanzo cha ugomvi wao ni Miss Tanzania wa mwaka 2006, Wema Sepetu ‘Madam’.

Akizungumza leo Novemba 24, 206 wakati wa mahojiano kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM, Dimpoz amesema mwanzoni walikuwa na urafiki mzuri na Diamond na walikuwa wakishirikiana mambo mengi kuhusu muziki wao, lakini baadaye hali ilikuwa tofauti baada, Diamond akaanza kumpoteza na kukwepa kufanya naye baadhi ya mambo kwa pamoja.

Dimpoz amesema hayo baada ya Diamond kusema mambo kadhaa kuhusu yeye wakati akifanya mahojiano jana kwenye kipindi hicho cha XXL.

Haya ndiyo maneno ya Ommy Dimpoz:

“Mimi nimefahamiana na Diamond miaka mingi kabla hajatoa hata wimbo wake wa Kamwambie.

“Diamond aliwahi kuniambia kuwa inabidi tuwe makini kwa sababu kuna watu wanasema mimi nakupeleka kwa waganga wangu.

“Lakini ilifika mahali nikaona kama anaanza kunikwepa.

“Kuna wakati hata nilipokuwa nikumuuliza kama anasafiri alisema hapana lakini unashangaa anapost picha yuko sehemu fulani.

“Nilimuomba twende wote AFRIMA Marekani akakubali, nilimwambia nitagharamia, lakini kila nikimuuliza safari lini hasemi.

“Siku nyingine nampigia simu hapatikani, alipopatikana yupo Afrika Kusini anaenda kwenye tuzo Marekani anasema ni ghafla.

“Mimi nilikuwa naonekana kama mzigo kwa Diamond, lakini sikujali maneno ya watu sababu nilijua nilipotoka naye.

“Mimi nilipanga kufanya ngoma na Iyanya (wa Nigeria) alipokuja Dar es Salaam, lakini nakuja kushtuka nakuta Diamond tayari amesharekodi naye.

“Mimi sikuwahi kugombana na Diamond, ni vitu vimetokea unaona tu mwenyewe kuwa hapa sitakiwi, unaamua kurudi nyuma.

“Baada ya choko choko zote, nilipo ‘shoot’ video ya Wanjera na kumuweka Wema (Wema Sepetu) ndio balaa lilipoanzia hapo.

“Mimi sikumweka Wema Sepetu kwenye wimbo wangu kwa makusudi, lakini ana amashabiki wengi na niliona hii itanisaidia.

“Wema ni rafiki yangu kitambo kabla hajaanza uhusiano na Diamond. Na walivyo-‘kiss’ mara ya kwanza kwenye gari nilikuwepo

“Mimi kuna wakati nilikuwa namuomba ata anitambulishe kama msanii wake kwa wasanii wakubwa ili tu nipate ‘connection’.

“Nashangaa kwanini Diamond achukie mimi kuwa karibu na Wema, mbona anaongea na wengine waliokuwa karibu naye, kwanini mimi?

“Mimi sina timu kwenye mitandao, labda mashabiki zangu tu, lakini sina timu yenye kazi ya kutukana au kubishana mitandaoni.

“Mimi sijali Diamond alivyonitukana, au wanaosema mimi shoga. Kikubwa nachoshukuru najijua kuwa mimi mzima, so sijali.

“Kuna wakati simu ilipigwa kutoka Sweden nikatumbuize, lakini Diamond alisema mimi nina nyimbo mbili na kutumbuiza sijui.

“Kuna wakati nilikuwa sina hela ya kutoa wimbo, nikamwambia Diamond anisimamie nitoe wimbo lakini hakufanya hivyo

Hata hivyo Dimpoz hakusita kumtuhumu Meneja wa Diamond, Sallam.

“Baada ya kuzungumzia ishu ya ‘viewers’, Sallam aliniambia kua kati ya vitu nilivyomuuzi ni kuzungumzia hilo.

“Nilipopost ‘insta’ kuhusu watu kununua ‘views’ YouTube, sikumtaja mtu, nilisema tu sasa hivi watu wanaweza.

““Baada ya kupost ‘insta’ kuwa kuna wasanii wananunua ‘views’ YouTube, nilikutana na meneja wa @diamondplatnumz, Sallam

“Meneja @Sallam_SK amekuwa akitaka mimi nimpigie Diamond simu tumalize, hata juzi ameniambia nikiwa na Shetta.

“Nikawa najiuliza kwanini @Sallam_SK kila mara ananitaka mimi ndio nipige simu, kwamba huyo mwingine ni ‘special’ sana?

“Mimi nilishamwambia Sallam kama anataka kutupatanisha, basi tukutane kwa AY kila mmoja aseme lake tuyamalize haya.

Kuhusu bifu la Ali Kiba na Diamond

“Kwenye wimbo wa Lala Salama wa Diamond, alitoa sauti ya Ali Kiba aliyokuwa ameingiza bila ya kumwambia Ali Kiba.

“Diamond na Ali Kiba walikuwa marafiki wakubwa, ila kitendo cha Diamond kutoa sauti ya Kiba bila kumwambia kilimkera sana.

Dimpoz akubali yaishe.

“Sisi tunahangaika kuwa kama Wanaijeria lakini wao tayari wamehama. Ukimsikiliza Wizkid anafanya vitu tofauti kabisa.

“Tunataka kuwapita Wanaijeria, lazima tushirikiane kwa sababu wao wapo pamoja na wanazidi kwenda mbali.

“Haya mabishano/bifu kwenye mziki ziwepo, ila ziwe na lengo la kujenga, tubishane kuhusu muziki na tutengeneze pesa wote.

“Mimi nimechangia kwa kiasi kikubwa kuandika wimbo wa Nasema Nawe wa Diamond, lakini sikuwahi kusema wala kutaka ‘credit’.

“Mimi nilimsadia kuandika sio kwamba yeye hajui, lakini ni kawaida ya wasanii kusaidiana hasa wanapokutana studio.

“Naheshimu mawazo ya Diamond na kuutambua mchango wake kwangu, na wala sishindani naye.

“Mimi naongea ukweli, sina tatizo na mtu. Naamini Diamond anavyofanikiwa ndio njia ya kufanikiwa kwa wasanii wengine.

“Kuna vitu ambavyo mashabiki hawafahamu ukiendeshwa kwa jazba utakuwa haufiki popote mziki ni kushi.
“Mimi nilimsadia kuandika sio kwamba yeye hajui, lakini ni kawaida ya wasanii kusaidiana hasa wanapokutana studio.

“Uandishi wa nyimbo ya #NasemaNawe ya @diamondplatnumz verse ya pili mimi nimeiandika!

“Kama kuna ubaya Mwenyezi Mungu aniepushe na haya, Sina ubaya wowote na jamaa..!

Kuhusu aliyekuwa meneja wa Ommy Dimpoz, Mubenga

“Kuhusu mimi na Mubenga, alisema kuwa haoni faida ya kufanya kazi na mimi hivyo anataka kufanya kazi zake mwenyewe.

“Nilimsihi Mubenga abako, lakini akaamua kuondoka akidai kuwa mimi ni tajiri lakini yeye hapati faida.

“Meneja Mubenga alishawahi kuniambia mbele ya @Nedyboy2 ifike mwisho wa kufanya kazi pamoja wala sina ubaya naye.” Amesema Ommy Dimpoz.
Previous
Next Post »