Staa Ali Kiba amesema hajamkosea kitu Hakeem 5 na anashanga kusikia jamaa anasema ana chuki naye.
Stori
hii ilianza baada ya Abby Skills kusema Hakeem 5 lazima amuombe msamaha
Ali Kiba ili wafanye kazi tena na mambo yake yaende sawa.
Ali Kiba alisema “Kuhusu
Hakeem 5, naweza kusema kwanza ni ndugu yangu kama Abby Skills na
wengine. Tunaheshimiana nae sana. Sina ugomvi nae, tumefanya kazi nae
kwa mapenzi yote tulipokuwa lebo moja G-records
Kuhusu colabo na kutofanya video ya wimbo wa Hakeem 5 Kiba anasema “Ishu
ipo hivi, nakumbukuka kabla sijapumzika kimuziki kipindi kile tulifanya
kazi na Hakeem 5, nakumbuka ilikuwa inaitwa MADEBE. Baada ya kuitoa
ilifanya vizuri, then nikaamua kupumzika miaka mitatu. Niliporudi rasmi
akanifata tufanye video! Nikamwambia kweli?? Upo serious! Yani nyimbo
ina miaka, then tuifanye video kweli. Ni Unprofessional kwa kweli.”
Kuhusu kufanya nae colabo tena, Kiba aliniambia “Sitaki kufanya nae tena nyimbo, sijamkosea Hakeem lakini sitakuja kufanya nae kazi.”.
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon