Wanajeshi wa Japani.
10:
JAPAN Japan ilikuwa moja ya nchi vinara katika Vita ya Pili ya Dunia
(WW2) iliyomalizika mwaka 1945. Cha kufurahisha, baada ya vita hiyo,
Japan iliingia kwenye mkataba wa amani na kukubaliana kuwa na jeshi la
kawaida lakini kufuatia kukua kwa Jeshi la China ndipo ikaanza kupanua
tena jeshi lake ikiweka ngome za kijeshi kwenye visiwa vyake. Bajeti ya
Jeshi la Japan imekuwa ikiongezeka kila mwaka hadi kufikia Dola za
Kimarekani bilioni 49. Jeshi hilo lina zaidi ya wanajeshi 247,000
waliopo kazini na zaidi 60,000 wa akiba. Lina ndege za kivita zipatazo
1,595 na meli 131.Jeshi ni sehemu
muhimu ya nchi na usalama wake. Kila mwaka nchi hutenga bajeti kwa ajili ya kuimarisha majeshi yake. Nchi nyingi duniani huchukua tahadhari za kiusalama kwa kuimarisha majeshi yake kulinganisha na nchi nyingine zinavyofanya. Nchi hizo hufanya hivyo kwa kumiliki idadi kubwa ya wanajeshi, kuboresha teknolojia ya kijeshi, kutoa mafunzo na kutengeneza propaganda za kidiplomasia ili kuwaogopesha maadui wao wa kiusalama. Ngoja tuangalie majeshi kumi (Top 10) hatari duniani kwa sasa na bajeti zake;
muhimu ya nchi na usalama wake. Kila mwaka nchi hutenga bajeti kwa ajili ya kuimarisha majeshi yake. Nchi nyingi duniani huchukua tahadhari za kiusalama kwa kuimarisha majeshi yake kulinganisha na nchi nyingine zinavyofanya. Nchi hizo hufanya hivyo kwa kumiliki idadi kubwa ya wanajeshi, kuboresha teknolojia ya kijeshi, kutoa mafunzo na kutengeneza propaganda za kidiplomasia ili kuwaogopesha maadui wao wa kiusalama. Ngoja tuangalie majeshi kumi (Top 10) hatari duniani kwa sasa na bajeti zake;
Wanajeshi wa Korea Kusini wakifanya mazoezi.
9:
KOREA KUSINI Korea Kusini wanashirikiana mpaka na Korea Kaskazini ambao
nao wapo vizuri kijeshi. Ili kukabiliana na majeshi makubwa ya China
and Japan, Korea Kusini imekuwa ikiongeza bajeti ya jeshi lake hadi
kufikia dola bilioni 34. Lina wanajeshi waliopo kazini 640,000 na
wengine wa akiba 2,900,000. Lina ndege kubwa za kivita 1,393 na meli za
kijeshi 166.
Wanajeshi wa Uturuki.
8:
UTURUKI Labda ni kwa sababu ya kushirikiana kupambana na kundi korofi
la kigaidi la Islamic State linalotishia amani duniani ndiyo maana ni
kubwa na linaogopeka zaidi. Limeongeza bajeti yake kwa 10% hadi kufikia
dola bilioni 18. Lina wanajeshi wapatao 660,000 walioko kazini na wa
akiba. Pia lina ndege za kivita 1,000 na silaha za nchi kavu 16,000
likiwa lina ushirikiano mkubwa na lile la Marekani.
Wanajeshi wa Ujerumani.
7:
UJERUMANI Miongoni mwa nchi zenye majeshi hatari duniani ni Ujerumani.
Linatengewa bajeti ya dola bilioni 45, japokuwa linaonekana kushuka
katika miaka ya hivi karibuni labda kwa sababu kizazi cha sasa nchini
humo hakipendi mambo ya vita na watu wengi wanaogopa kujiunga na jeshi
hilo. Lina wanajeshi 183,000 walioko kazini na 145,000 wa akiba likiwa
na ndege za kivita 710 na silaha za nchi kavu zaidi ya 5,000.
Wanajeshi wa Ufaransa.
6:
UFARANSA Katika miaka ya hivi karibuni, Ufaransa imepunguza bajeti ya
jeshi lake hilo kwa 10%. Bajeti yake inafikia dola bilioni 43 kwa mwaka.
Lina wanajeshi 220,000 waliopo kazini na 500,000 wa akiba. Pia lina
ndege za kivita 1,000 na vifaa vya nchi kavu 9,000.
Waajeshi wa Uingereza.
5:
UINGEREZA Uingereza ni miongoni mwa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya
(EU) ambao wapo kwenye mkakata wa kupunguza wanajeshi wake kwa 20%.
Bajeti ya jeshi lake hatari ni dola bilioni 54 kwa mwaka likiwa na
wanajeshi 205,000, ndege za kivita 908 na meli 66.
Wananchi wa India wakiwa katika mazoezi.
4:
INDIA Jeshi lake lina jumla ya ‘wajeda’ milioni 3.5, wakiwemo milioni
1.325 waliopo kazini na wengine ni wa akiba. Lina magari ya kivita
16,000 na ndege 1,785 pamoja na silaha za nyuklia. Bajeti yake ni dola
bilioni 46.
Wanajeshi wa China.
3:
CHINA Bajeti ya Jeshi la China inafikia dola bilioni 126 likiwa na
wanajeshi milioni 2.285 waliopo kazini na milioni 2.3 wa akiba. Ni moja
ya majeshi makubwa kwa sasa duniani likiwa katika Tatu Bora. Lina vifaa
vya kivita vya nchi kavu 25,000 na ndege 2,800. Pia lina silaha za
nyuklia 300.
Wanajeshi wa Urusi.
2:
URUSI Bajeti ya jeshi hatari la Urusi ni dola bilioni 76.6 ambayo
inatarajiwa kuongezwa kwa 44%. Tangu alipoichukua Urusi, Rais Vladimir
Putin mwaka 2000, nchi hiyo imekuwa moto wa kuotea mbali katika masuala
ya kijeshi. Lina wanajeshi 766,000 waliopo kazini na milioni 2.5 wa
akiba. Urusi inaongoza kwa silaha za kivita zikiwemo za nyuklia zipatazo
8,500
Wanajeshi wa Marekani.\
1:
MAREKANI Jeshi kinara la Marekani linatengewa bajeti ya dola bilioni
612.5. Hakuna jeshi lenye bajeti kama hiyo duniani. Lina wanajeshi
milioni 1.4 waliopo kazini na 800,000 wa akiba. Hawa jamaa ni wabaya kwa
ndege, meli na manowari za kivita. Pia lina silaha za nyuklia 7,500.
Kama ulikuwa hujui ndilo jeshi namba moja duniani tangu Vita ya Pili ya
Dunia iliyomalizika mwaka 1945. Nchi kama Urusi na China zinangoja sana
kwa jeshi la Marekani kutokana na kuwa na mbinu na teknolojia ya hali ya
juu ya kijeshi. NB: Data kama hizi ni vigumu kuzipata kwa baadhi ya
nchi za Afrika. Imeandaliwa na Sifael Paul kwa msaada wa mtandao.
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon