SAKATA la Mwandishi Halfani Lihundi , Mkuu wa Mkoa wa Arusha Aingilia Kati

Sakata la mwandishi wa habari wa ITV Halfan Lihundi kukamatwa na kuwekwa mahabusu kwa saa 24 kwa amri ya mkuu wa wilaya ya Arumeru baada ya kuandika habari ambayo haikumfurahisha mkuu huyo, limechukua sura mpya baada ya mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kuingilia kati na kusema waandishi wa habari wanao uhuru wa kuandika habari mahali popote katika mkoa huo ili mradi wazingatie weledi katika taaluma.

Gambo ambaye wakati sakata hilo linatokea alikuwa safarini analazimika kukutana na wanahabari wote wa jiji la Arusha baada ya tukio hilo lililogoga vichwa vya waandishi mkoa wa huo na kusababisha kusimamisha shughuli zao ikiwemo kuweka kalamu chini kumnusuru mwenzao lakini pia wadau mbalimbali tasnia ya habari kukerwa na kitendo hicho.

Gambo amesema anatambua umuhimu wa kazi za waandishi wa habari na kuongeza kuwa kabla ya kiongozi huyo hajafanya maamuzi hayo pamoja na mamlaka aliyonayo busara ilitakiwa itumike.

Claud Gwandu ni mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa arusha na baadhi ya waandishi arusha anapaza sauti zao kuonyesha hisia zao juu ya sakata hili.

Lakini busara ya Gambo inatuliza munkari ya waandishi hawa na kumaliza mzozo huo ambao ulionekana kwenda mbali zaidi.

Na je nini kauli ya mkuu huyo kuhusiana na usalama wa waandishi hawa wakiwa katika kutekeleza majukumu yao?

Akiwa mkoani arusha katika majumuisho ya ziara yake mwishoni mwa wiki iliyopita waziri mkuu aliwapongeza waandishi wa habari kwa kazi nzuri ambayo wamekuwa wakiifanya kwani huamsha au hutoa mrejesho wa mambo muhimu ambayo huwasaidia viongozi kufanya maamuzi sahihi.
Previous
Next Post »