Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Projestus Rwegasira
amewasilisha taarifa ya utekelezaji wa maagizo ya Bunge ya kuhakikisha
mfumo wa vifaa vya utambuzi wa alama za vidole unafungwa katika wilaya
za kipolisi 108 nchi nzima kwa muda wa miezi mitatu.Zabuni ya kufunga na
kusambaza mashine hizo za utambuzi wa vidole katika Jeshi la Polisi
ulifanywa na Kampuni ya Lugumi.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti
wa kamati hiyo Naghenjwa Kaboyoka, aliwathibitishia waandishi wa habari
mjini Dodoma jana kuwa ripoti hiyo tayari imekabidhiwa kwa Ofisi ya
Spika wa Bunge, Job Ndugai.
Kaboyoka alisema ripoti hiyo baada ya kukabidhiwa kwa Spika Ndugai ataipitia na baadaye kuiwasilisha kwa kamati hiyo ya PAC.
Juni 30, mwaka huu,
Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson baada ya kuahirisha Bunge la
Bajeti aliiagiza serikali kuhakikisha mfumo huo unafanya kazi kwa ajili
ya kuwadhibiti wahalifu na kuitaka Kamati ya PAC ifuatilie suala hilo.
Dk Tulia alitoa agizo
hilo baada ya kupokea taarifa yenye utata ya kuhusu zabuni yenye thamani
ya Sh bilioni 37 ya kufunga mashine hizo katika vituo vyote vya Polisi
baina ya Jeshi la Polisi na Kampuni ya Lugumi Enterprises Limited
iliyotolewa mwaka 2011.
“Ninashauri serikali
ihakikishe mradi huu unakamilika ndani ya kipindi cha miezi mitatu
kuanzia leo…, mradi huu utasaidia Jeshi la Polisi kuwatambua kwa haraka
watu waliohusika katika matukio ya uhalifu mbalimbali,” alisema.
Katika mkataba huo,
Lugumi inatakiwa kusambaza na kufunga mashine hizo za utambuzi wa vidole
katika wilaya 108 za kipolisi nchi nzima.
Hata hivyo, mashine hizo
zilifungwa kwenye vituo 14 pekee wakati tayari kampuni hiyo ilishapokea
kiasi cha asilimia 99 za malipo yake.
Katika ripoti ya Mkaguzi
na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka wa fedha 2013/14
ilionesha kuwa pamoja na kampuni hiyo ya Lugumi kulipwa asilimia 99 ya
malipo sawa na Sh bilioni 34, bado haijakamilisha mradi huo kwa muda wa
miaka mitano sasa.
Aprili, mwaka huu, PAC
iliunda kamati ndogo kwa ajili ya kuchunguza mkataba huo wa utata baina
ya Kampuni ya Lugumi na Jeshi la Polisi.
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon