Maddie
Ziegler ni msichana wa miaka 14 ambae kwa mara ya kwanza alionekana
kwenye TV Show iliyokua ikiitwa Dance Moms. Umaarufu wake ulizidi
kuongezeka mara baada ya mtoto huyo kujiingiza kwenye fani ya uchezaji
muziki (Dancer) kama umeiona Chandelier ya Sia utakua umemuona mtoto
huyu michezo aliyotisha nayo humo.
Ziegler alikua jaji kwenye msimu wa sita wa shindano la So You Think You Can Dance:
Michelle
Obama anatajwa kama moja kati ya wanawake wahamasishaji na wapenda
maendeleo kwa sasa anaungana na binti yake Sasha kuendelea kuelimisha
wanawake waelimike, Malia Obama anatarajia kujiunga na chuo kikuu cha
Havard.
Barack Obama ambae ni Baba yao mzazi ameshikiria rekodi ya kuwa Rais wa kwanza mweusi nchini Marekani..
Malia na Sasha Obama pia hawajasahaulika kwenye orodha hii ya mastaa wenye umri mdogo na ushawishi mkubwa duniani.
Miaka
nane sasa baada ya ushindi wake kwenye Tamasha la America’s Got Talent,
Zara ni mmoja kati ya watoto wanaosumbua sana kwenye muziki wa Pop. Kwa
miaka ya hivi karibuni Zara amezidi kujizolea umaarufu baada ya
kusikika kwenye ngoma kadhaa zikiwemo “Never Forget You”
aliyoshirikishwa na MNEK na ile ngoma ya kombe la Euro “This One For
You” ya mtu mzima David Gueta.
“Ain’t
my fault” ndiyo ngoma ya mrembo Zara iliyoko kwenye chati kwa sasa kwa
mujibu wa mitandao mbalimbali ya kijamii ngoma hiyo imetajwa kama ngoma
inayomjenga zaidi mtoto wa kike na wanawake wengi ambao wamepata nafasi
ya kuisikiliza.
Mtoto
wa muigizaji Will Smith ambae haishiwi vituko na moja kati ya maajabu
yake ni uvaaji wake wa mavazi yake ya kike ambayo yamefanya jina lake
kuzidi kutajwa kwenye Industry ya Fashion…
Akiwa
na umri wa miaka 18 Jaden Smith tayari amezindua brand yake ya mavazi
inayoitwa MSFTSrep nguo maalum kwa wasichana wenye tabia za kiume
(TomBoy) au wavulana wanaopenda kuwa na muonekano wa kike.
2016
umekua ni mwaka wa kismati kwa girlfriend wa mnyamwezi Tyga kwani Licha
ya Staa huyo wa TV Show ya “Keeping Up With The Kardashians” kumiliki
mijengo na magari ya kifahari mrembo Kylie Jenner anamiliki kampuni yake
ya vipozi (Kylie Cosmetics) pia ameonekana kwenye kurasa mbalimbali za
majrida makubwa likiwemo Allure Magazine.
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon