Bondia Thomas Mashari ameuawa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo.

BONDIA
wa ngumi za kulipwa nchini Thomas Mashali ‘Simba asiyefugika’ ameuawa
usiku wa kuamkia leo na watu wasiojulikana na mwili wake umeokotwa
maeneo ya Kimara kabla ya kupelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Rais
wa Oganizesheni ya Ngumi za kulipwa (TPBO) Yassini Abdallah ‘Ustadh’
alisema mauti yalimkuta bondia huyo baada ya kupigwa na watu
wasiojulikana na mwili wake kuokotwa na wasamalia wema maeneo ya Kimara.
“Ni
kweli Mashali amefariki dunia nimepokea Habari hiyo muda mfupi uliopita
sasa nipo njiani naelekea Muhimbili” alisema Ustadhi.
Taarifa za utaratibu wa mazishi zitatolewa baadae na ndugu wa marehemu.
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon