Tamasha kubwa la muziki
la Fiesta linaelekea ukingoni, kwenye show ya mwisho ambayo huwa kubwa
zaidi ikiwakutanisha wasanii mbalimbali kwenye steji moja.
Wakali wa muziki wa
Afrika, Yemi Alade, Tekno na Jose chameleone ni baadhi ya wasanii wa nje
watakao shambulia jukwaa la tamasha hilo, huku tukiendelea kusubiri
msanii wa Marekani kutangazwa kama ilivyo desturi ya tamasha hilo.
Pia Tamasha la burudani
la Fiesta 2016 limekanusha taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ya
kijamii kwamba watamleta msanii wa Marekani Jay Z katika show ya Fiesta
Dar es salaam.
Mapema Jumamosi hii
zilisambaa picha ‘fake’ inayomuonyesha msanii huyo mahiri duniani akiwa
ameshasajiriwa kwa ajili ya tamasha hilo linalotarajiwa kufanyika
Novemba 5 katika viwanja wa Leaders Club jijini Dar es salaam.
Kupitia ukurasa wa instagram wa Clouds FM umetoa taarifa hii:
Kumetokea uzushi kwamba
tumemsajili msanii Jay Z kwa ajili ya kilele cha #Fiesta2016 hapo
#November05. Tunapenda kukanusha habari hiyo; picha iliyotengenezwa
kueneza habari hiyo ni batili.
Hii ni list ya wasanii wa Tanzania.
1. Ben Pol
2. Nandy
3. Christian Bella
4. Fid-Q
5. Weusi
6. Roma
7. Chegge
8. Dogo Janja
9. Billnass
10. Stamina
11. Jux
12. Barnaba
13. Maua Sama
14. Darassa
15. Vanessa Mdee
16. Sholo Mwamba
17. Jay Moe
18. Msami
19. Juma Nature
20. Snura
21. Baraka Da Prince
22. Shilole
23. Manfongo
24. Belle 9
25. Lord Eyes
26. Young Dee
27. Raymond
28. Mr. Blue
29. Alikiba – Kingkiba
30. Hamadai
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon