Scorpion (aliyefungwa pingu) akielekea kwenye chumba cha mahakama.
Scorpion akiwa ndani ya gari la polisi.
Ile
kesi inayomkabili Salumu Njwete ‘Scorpion’ ya kupora na kumjeruhi
sehemu mbalimbali za mwili, Said Mrisho, inatarajiwa kuanza kusikilizwa
rasmi Novemba 30, mwaka huu.
Akizungumza
leo wakati akimsomea mashtaka Scorpion alipopandishwa kizimbani kwa
mara nyingine katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, mwendesha mashtaka
Chensesia Gavyole mbele ya Hakimu Flora Haule alisema upepelezi wa kesi
umekamilika hivyo akamuomba hakimu ataje tarehe nyingine kwa ajili ya
kuanza kusikilizwa.
Hakimu
Haule alisema kesi hiyo inatarajiwa kuanza kusikilizwa Novemba 30,
mwaka huu lakini Scorpion alitoa ombi kwa mahakama kwamba kutokana na
kwamba upepelezi umekamilika asomewe maelezo ya awali hapohapo jambo
ambalo hakimu alimwambia haliwezekani mpaka siku hiyo kesi itakapoanza
kusikilizwa.
Septemba
6 mwaka huu maeneo ya Buguruni, Scorpion anadaiwa kuwa alimpora Said
fedha, cheni ya dhahabu na kumjeruhi kwa kisu sehemu mbalimbali za mwili
wake ikiwemo tumboni na begani ambapo kesi hiyo imekuwa ikitajwa mara
kadhaa mahakamani hapo.
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon