






Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akihutubia wakazi wa kijiji cha Kagunguli wilayani Ukerewe na kusisitiza serikali ya awamu ya tano ni ya kufanya kazi kwa bidii ili kuleta maendeleo ya Tanzania.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akihutubia wakazi wa kijiji cha Kagunguli wilayani Ukerewe.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akiwasalimia wakazi wa Nansio waliojitokeza kwa wingi kutaka kumsalimia na kuwakilisha kero zao wakati wa ziara yake katika wilaya ya Ukerewe
..................................................................
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameweka jiwe la
msingi katika mradi mkubwa wa maji kwenye mji Nansio katika kisiwa cha Ukerewe
mkoani Mwanza mradi ambao utahudumia wananchi elfu 61.
Makamu wa
Rais ambaye amesafiri kwa takribani masaa Matatu na meli ya MV Nyehunge II katika
Ziwa Victoria kwenda kisiwa Ukerewe kwa mara ya kwanza tangu ashike wadhifa
huo,amewahimiza wananchi hao wautunze mradi huo ambao utasaidia kwa kiasi
kikubwa kuondoa tatizo na uhaba wa maji safi na salama katika kisiwa hicho.
Mradi huo ambao
unaojumuisha kazi za uboreshaji wa huduma ya majisafi na usafi wa mazingira unatekelezwa
chini ya umefadhili wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na serikali ya Tanzania katika miji ya Sengerema,Geita na
Nansio – Ukerewe kwa gharama ya Dola za Kimarekani milioni 30.4 ambapo serikali
ya Tanzania imechangia mradi huo Dola za Kimarekani milioni nne.
Makamu wa
Rais Samia Suluhu Hassan amewaahidi wananchi kuwa serikali ya awamu ya Tano unamikakati
mizuri inayolenga kuondoa tatizo la maji kote nchini ili kusaidia wananchi hao hasa wanawake kutumia
muda mwingi kufanya kazi za maendeleo kuliko kutafuta maji.
Akihutubia mamia
ya wananchi wa kisiwa cha ukerewe kwenye
kijiji cha Kagunguli mkoani Mwanza mara baada ya kuweka mawe ya msingi katika
miradi miwili ya ukiwemo mradi wa maji na ujenzi wa chumba cha upasuaji katika
kituo cha afya cha Kagunguli, Makamu wa Rais amewapa pole wananchi wa kisiwa
hicho baada ya kukumbwa na tufani ya kimbunga cha upepo iliyotokea tarehe 04 Novemba
2016 na kusababisha uharibifu mkubwa ikiwemo nyumba za watu kubomoka.
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon