Meya
wa mji wa Clay nchini Marekani, Beverly Whaling amejiuzulu wadhifa huo
baada ya kuunga mkono maandishi yenye ubaguzi wa rangi kwenye facebook
dhidi ya mke wa Rais Barack Obama, Michelle Obama.Meya huyo aliingia
matatani na kuamua kujiuzulu nafasi yake baada ya kuonesha kufurahishwa
na ‘post’ ya kibaguzi iliyoandikwa na Mkurugenzi wa shirika moja la
kutoa misaada, Pamela Taylor aliyelenga kubainisha tofauti kati ya mke
wa Rais Mteule wa Marekani, Donald Trump, Melania na mama Michelle
Obama.
Taylor alimtusi Michelle akimfananisha na sokwe huku akimpamba Melania kuwa ni mrembo.
Meya huyo aliandika chini ya ujumbe huo wa kibaguzi, “Just made my day Pam.”
Zaidi
ya watu 200,000 wamejiandikisha mtandaoni ndani ya muda mfupi kupinga
ubaguzi huo na kuwataka Whaling na Taylor kujiwajibisha haraka.Vitendo
vya kibaguzi vimeripotiwa kuongezeka nchini humo tangu Trump
alipotangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais.
Ingawa
kauli zake wakati wa kampeni zilikuwa na matamko tata, Trump amewataka
wafuasi wake kuacha mara moja vitendo vyovyote vya kibaguzi akisisitiza
kuwa yeye atakuwa rais wa Wamarekani wote.
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon