Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa, Sospeter Muhongo amesema kuwa watanzania
wamechoka kukatika katika kwa umeme na huku akiwaambia Tanesco kuwa
Watanzania wanataka umeme wa bei nafuu.
Akizungumza
Jumatano hii Waziri huyo wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Uboreshaji wa
Miundombinu ya Umeme katika Jiji la Dar es Salaam alisema “Hatutaki mgao
wa umeme, naomba niwaeleze Tanesco hatutaki mgao wa umeme la kwanza
hilo, la pili Watanzania wamechoka na kukatika katika kwa umeme,
hatutaki kuona umeme unakatika katika, la tatu ili tujenge nchi ya
viwanda tunahitaji umeme wa uhakika narudia umeme wa uhakika , umeme
unaotabirika na wa bei nafuu,” alisema Muhongo.
Nae Mkurugenzi mkuu wa Shirika
la umeme Tanzania (Tanesco), Felschimi Mramba amesema mradi huo
umejengwa kwa msaada wa serikali ya Finland kwa kushirikiana serikali ya
Tanzania.
“Utekelezaji wa mradi huu
umehusisha pia ujenzi wa kuunganisha vituo vyetu vyote vilivyopo katika
ya jiji, vituo vya city centre, Kariakoo, Stesheni, Sokoine pamoja na
Ilala na hivyo kufanya kuwepo kwa mfumo unaosaidiana pale upande mmoja
unapokuwa hauna umeme,”alisema Mramba.
Siku za hivi karibuni Tanesco walitoa taarifa ya kuomba kupandisha bei ya umeme kwa asilimia 18.19.
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon