Mwanzilishi
wa THT na Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa Clouds FM, Ruge
Mutahaba, amesema licha ya Ruby kuwa na tofauti naye na kujiondoa kutoka
kwenye usimamizi wake, hawezi kushuka kimuziki sababu ana kipaji cha
hali ya juu.
Miezi
miwili iliyopita, Ruby alijiondoa kwenye usimamizi wa THT na kukataa
kutumbuiza kwenye tamasha la Fiesta hali iliyotafsiriwa kuwa hilo
linaweza kuwa anguko lake. Hata hivyo bado muimbaji huyo anaendelea
kuwika ikiwa ni pamoja na kushiriki kwenye kipindi cha Coke Studio
Africa ambako amejinyakulia sifa za kutosha.
Akiongea
na mtangazaji wa Mashujaa FM ya Lindi, Baby Dinny, Ruge amesema kipaji
cha Ruby ni ‘unstoppable’ na kwamba kama akipata waandishi wengine
wazuri atafika matawi ya mbali.
“Mimi
naamini Ruby ana kipaji sana. Binafsi ana kipaji cha ukweli kabisa wala
sio uongo,” alisema Ruge. “Kama atashuka labda itakuwa ni mambo yake tu
mwenyewe lakini sidhani kama kuna namna kipaji chake kitashuka,”
aliongeza na kumshauri kuwa apate watunzi wengine wazuri wa kumsaidia.
Anadai kuwa nyimbo zake tatu, Na Yule, Forever na Sijutii, ziliandikwa
na yeye akishirikiana na Amini na Barnaba.
Kwa
upande mwingine, Ruge amesema haoni kama kuna tatizo Ruby kuondoka THT
kwakuwa tofauti na wengine wanavyodhani, THT si label bali ni kama chuo
ambacho wasanii mbalimbali hunolewa.
“Yeye
ameona yuko tayari kivyake kwenda kwenye sehemu anayoweza kupata
maslahi zaidi, ndio hivyo tu, kwahiyo sioni kama kuna shinda,”
amesisitiza Ruge.
Pia
amedai kuwa muda wowote ambao muimbaji huyo atahitaji ushauri kutoka
kwake, milango iko wazi kwakuwa bado ataendelea kumchukulia kama mdogo
wake.
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon