Msanii
Ommy Dimpoz amekanusha tetesi za kuwa na ugomvi na aliyekuwa 'business
partiner' ambaye pia alikuwa meneja wake maarufu kwa jina la Mubenga,
baada ya kila mmoja kuchukua hamsini zake na kufanya yake.
Akizungumza
kwenye FNL ya East Africa Television Ommy Dimpoz amesema Mubenga
ameamua kufanya biashara zake mwenyewe bila kushirikiana naye, kitu
ambacho ni jambo zuri kwake na kwa maendeleo pia, lakini hawana tofauti
na hata akihitaji msaada wake, yupo tayari kumsaidia.
"Mubenga
ameenda kuanzisha kitu chake, hiyo ni pongezi na hayo ni maendeleo,
mnataka kila siku awe chini ya Ommy! yeye ameenda kuazisha kitu chake,
kampuni yake, ana wasanii wake anawasimamia, anajua kwamba afanye vipi
anahitaji ku'move on', kwa hiyo ilikuwa ni movement yake yeye kwamba
ameamua kufanya kazi zake mwenyewe which is good, na mimi hata leo
akisema Ommy nataka suport hii kwa wasanii wangu i'm ready", alisema
Ommy Dimpoz.
Ommy
Dimpoz amesema hata tetesi za kuchukua hela za Mubenga na gari hazina
ukweli wowote, ni maneno tu ya uzushi ya mashabiki, na bado anamchukulia
kama ndugu yake.
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon