Joh Makini ameweka wazi kuwa hafanyi muziki mzuri kwa kuangalia kuja kuwa nominated kwenye tuzo flani.
Joh Makini
Rapa
huyo kutoka kwenye kundi la Weusi, amezungumza hayo baada ya kuwepo kwa
maswali mengi kuwa mbona hajatajwa kuwania Tuzo za kimataifa zikiwemo
MTV kwa mwaka huu ilihali akiwa na ngoma kali kama Don’t Bother aliyo
mshirikisha AKA kutoka Afrika kusini.
Lakini
pia Joh ameweka wazi kuwa juhudi zake sio muziki wa Afrika Mashariki
tu, Ni muziki wa Dunia na ana amini amefanya vitu vichache sana japokuwa
watu wanaona amefanya vitu vikubwa huku yeye akipanga kufanya muziki
mzuri zaidi na mkubwa.
Tutarajie makubwa mengi kutoka kwa Rapa Joh Makini kwenye muziki wake.
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon