NAIJUA familia ya mboga
saba? Wengine wanapenda kuwaita watoto wa kishua ama familia bora. Hii
ikiwawakilisha watoto wanaozaliwa kwenye familia yenye uwezo mkubwa wa
kiuchumi, kiasi cha kutumia mlo mmoja ukiwa na mboga tofauti na
zinazobadilishwa kila uchao. Ndio, kuna familia nyingine bhana mlo
unakuwa na mboga moja na huwa ni hiyo hiyo deile mpaka inachosha.
weeIngawa kuna dhana
kuwa watoto wa kishua huwa wavivu kujitafutia kwa sababu kila
anachokotaka hukipata tu nyumbani, lakini ukweli sio wote. Kuna wengine
wanaamua kuchakarika kutafuta maisha yao wenyewe, hata hawalingani na
wale waliotokea familia za watu duni ambao walikatisha masomo ili kusaka
noti wakiwa kwenye umri mdogo kabisa.
Mwanaspoti inakuletea
baadhi ya mastaa wa kike waliozaliwa kwenye familia ya mboga saba,
lakini wanakomaa kivyao vyao ile mbaya wakijichanganya na wenzao kusaka
noto kwa jasho na damu.
VANESSA MDEE
Vanessa Mdee maarufu
kama Vee Money alizaliwa mjini Arusha mwaka 1988. Vanessa anatokea
familia bora ya Sammy Mdee ambaye kwa sasa ni marehemu. Enzi za uhai
wake, baba ya Mzee alikuwa mtu mzito kwenye nchi hii akiwa mume wa
Sophia.
Akiwa na umri mdogo
Vanessa aliweza kusafiri nchi mbalimbali duniani. Vanessa Mdee alikulia
miji ya New York , Paris, Nairobi na Arusha, lakini kwa sasa jamaa
anatisha mbaya kwenye fani ya muziki akitamba ndani na nje ya Afrika.
JOKATE MWENGELO
Huyu unaweza kumuita mtoto wa Oysterbay kwani ndio alipokulia huku baba yake akifanya kazi serikalini.
Kumbuka Jokate alizaliwa
Washington DC, Marekani ambapo wazazi wake walikua wakifanya kazi huko.
Alipomaliza masomo ya juu ya Sekondari pale Loyola ndipo alipoanza
kujichanganya kwa kuwania taji la Miss Tanzania mwaka 2006 na kushika
nafasi ya 2 nyuma ya Wema Sepetu, kisha kuhamia kwenye fani ya muziki,
utangazaji, mitindo na ubunifu na sasa akipiga fedha.
WEMA SEPETU
Wema Sepetu ni msichana
anayetoka kwenye familia ya kibalozi akiwa ni mtoto wa mwisho katika
familia ya wasichana wanne wa marehemu Balozi Isaac Sepetu.
Wema alizaliwa mwaka
1988 katika hospitali ya St. Andrew ya Dar es Salaam na amesoma elimu
yake ya awali mpaka sekondari kwenye Shule ya Academic International
iliyopo Dar es Salaam kabla ya kwenda Malaysia kusomea mambo ya biashara
za kimataifa katka Chuo Kikuu cha Limkokwing.
Alianzia shindano la
urembo akitwaa mataji kadhaa ikiwamo la Miss Tanzania 2006 kisha kuhamia
kwenye filamu na sasa anaendelea kukimbiza akimiliki kampuni yake na
akizalisha bidhaa zenye jina lake. Achana kabisa, ila ukiamua kubisha we
bisha tu.
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon