
Muda
mfupi baada ya Timu yake ya mpira wa kikapu ya Gloden State Warriors
kuifunga timu yake ya zamani kwa pointi 26, Novemba 3, Kevin Durant
alikuta na Hasheem Thabeet ambaye aliwahi kuwa nae katika timu moja ya
Oklahoma City Thunder ambaye alikuwa natafuta kazi. Wote waliwahi kuwa Na. 2 kuchaguliwa kwenye orodha ya NBA draft za mwaka 2007 na mwaka 2009.
Wakati Durant alikuja juu na kuwa superstar, Thabeet hakuwahi kuweza
kufikia hatua hiyo, akiwa ametokea chuo cha Connecticut, na kucheza
katika timu nne za NBA na tatu za D-League kabla ya kuwa mchezaji ambaye
yuko huru kucheza timu yeyote nab ado hajachukuliwa na timu yeyote
mpaka mwaka 2015.
Durant bado anamatumaini makubwa na Hasheem na kwamba ipo siku atapewa nafasi.
Kwa maneno yake alisema: ‘Hasheem anajua hamna mtu anayemuonea huruma,
na wala yeye mwenyewe hajionei huruma, yeye ni ni mmoja wa wachezaji
wenye juhudi na pia ni mtu mzuri sana, na ni mmoja kati ya mchezaji
mwenza mzuri sana kuwahi kuwa nao karibu. Ipo siku atapata nafasi, kwa
sasa anajaribu kuwa mvumilivu’.
Baada ya kuumia kwa hisia zake aliposhindwa kuendelea NBA, Thabeet
mwenye umri wa miaka 29 sasa, anaamini kwamba, mwili wake, akili yake na
uwezo wake kimchezo umeshapikwa na kuiva sasa baada ya kuenda San
Francisco kufanya mazoezi na Frank Matrisciano na Meneja wa zamani wa
NBA, Milt Newton mwishoni mwa mwezi Aprili.
Thabeet aliongelea kujifunza kwake mpira wa kikapu tangu akiwa na miaka
15 hapa nchini Tanzania mpaka kufikia kuchaguliwa kuwa Na. 2 kwenye
draft ya NBA na mpaka baadae kufeli kabisa.
Kwa sasa Hasheem anaamini bado umri wake unaruhusu, alipokua kiakili
mwkaa jana ni tofauti na alipole hii, mazoezi anayofanya mniji San
Francisco yamemsaidia sana kutengeneza mwili na kuchonga kiakili, ana
imani sana na mwalimu wake wa mazoezi.
Ameamua kubakia nchini Marekani kuendelea na mpira huo wa kikapu. Anajua wazi Watanzia tunamuangalia na tunamuamini sana.
Alipoulizwa ni kitu gani ambacho angeweza kufanya tofauti katika kipindi
chote alichochezea Ligi ya NBA, alisema angeendelea kuwa mtulivu kama
livyokuwa na kufanya kile tu alichopswa kufanya. Na cha zaidi angeliomba
kuuliza au kuambiwa sababu kwanini hawakuendelea naye tena. Kwani
kitendo cha kumuengua mtu bila kusema wapi amekosea, hakumjengi
mchezaji.
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon